HABARI MBAYA KWA YANGA, WAPULIZIWA DAWA KWENYE VYUMBA VYA KUBADILISHIA NGUO

Wachezaji wa Yanga wamegomea kuingia katika vyumba vya kubadilishia nguo kwa madai kwamba kumepulizwa dawa ya kuwapunguza nguvu kwenye Uwanja wa Samora, Iringa.

Wachezaji wa Yanga waliingia uwanjani kwa miguu wakitumia geti kuu (geti la kuingilia viongozi) na basi lao limeingia likiwa tupu.

Hata hivyo wachezaji na benchi la ufundi hawaingia kwenye chumba kubadilishia nguo na wamekaa nje ya chumba hicho huku baadhi ya viongozi wa Yanga wakionekana kuingia na kutoka chumba hicho.

Meneja wa Yanga, Saleh Hafidh alisema chumba wanachotakiwa kubadilishia nguo wachezaji wao kimepuliziwa dawa hivyo wamegoma kukitumia.

“Hatuwezi kuingia katika chumba hiki kilichopuliziwa dawa, kama vipi tupewe chumba cha Lipuli na wao waje kwetu,” alisema Hafidh.

Hata hivyo madai hayo yalipigwa na Meneja wa Uwanja wa Samora-Iringa, Lazaro Manila alisema madai ya chumba chao kupiliziwa dawa yenye harufu mbaya siyo kweli.
“Hawa wameingiwa hofu inayoambatana na imani potofu za kishirikina na wanachokitafuta ni kupigwa faini tu ya kugoma kuingia ndani,” alisema Manila.

Nayo timu ya Lipuli imeingia uwanjani kwa kutumia geti kuu la kuingilia viongozi na kuliacha basi la kuingia uwanjani likiwa tupu.

Post a Comment

0 Comments