HII NDIO KAZI KUBWA WALIYONAYO WACHEZAJI WA KLABU YA YANGA LEO JUMATATU FEBRUARI 12,2018

Baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya St Louis kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa juzi, kikosi cha Yanga kinatarajiwa kuendelea na mazoezi leo Jumatatu kujiandaa na mchezo wa ligi unaofuata dhidi ya Majimaji katika raundi ya 18.

Mchezo huo unatarajiwa kupigwa kwenye uwanja wa Taifa Jumatano ya February 14 mwaka huu kuanzia saa 16:00 jioni.

February 21-2018, Yanga inatarajiwa kuelekea Shelisheli wiki moja baadae kwa ajili ya mchezo wa marudiano na Saint Louis.
Kikosi hicho kilipewa mapumziko ya siku moja (jana Jumapili) baada ya mchezo wa juzi Jumamosi February 10.

Post a Comment

0 Comments