HIVI NDIVYO SIMBA WALIVYOENDELEA NA MAZOEZI YAO JANA JIONI

Kikosi cha Simba jana jioni kimeendelea na mazoezi kwenye uwanja wa Boko jijini Dar es salaam kujiandaa na mchezo ujao dhidi ya Azam Fc.


Simba inajiandaa na mchezo wa ligi kuu ya Vodacom dhidi ya Azam FC, mchezo utakaopigwa kesho Jumatatano ya February 07 kwenye uwanja wa Taifa.

Habari njema ni kurejea kikosini kwa mshambuliaji Emanuel Okwi na golikipa nambari mbili wa Simba Said Mohamed 'Nduda'

Okwi aliumizwa juzi kwa kupigwa kiwiko cha makusudi na mlinzi wa Ruvu Shooting Mau Bofo na sasa amerejea na kuungana na kikosi hicho kilichofanya mazoezi jioni ya jana katika uwanja wa Book uliopo Dar es salaam.

Pamoja na kurudi kwa Okwi pia golikipa namba mbili wa klabu hiyo Said Mohamed 'Nduda' amerejea kutoka kwenye majeraha aliyoyapata akiwa mazoezini Zanzibar kwenye maandalizi ya mechi ya watani wa Jadi Young Africans.

Kurejea kwa 'Nduda' kunapunguza idadi ya majeruhi wa klabu hiyo kubakia mmoja tu Haruna Niyonzima.

Mchezo wa Simba dhidi ya Azam FC una umuhimu wake, ushindi utaiweka Simba mbele kwa tofauti ya alama nane dhidi yao.

Chanzo - nijuzehabari.co.tz

Post a Comment

0 Comments