SERIKALI YATOA ONYO KALI KWA WANAWAKE WANAOKUZA MAUMBILE YA MIILI YAO

Serikali kupitia Wizara ya Afya, Jisnia, Wazee na Watoto imewaonya wanawake wanaotumia dawa za aina mbalimbali kukuza sehemu za maumbile ya miili yao na kusema kuwa wanajiweka katika hatari kupata matatizo mbalimbali ya kiafya.

Hayo yalisemwa jana bungeni mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Afya, Dkt Faustine Ndungulile wakati wa akijibu swali katika kipindi cha maswali na majibu bungeni.

Dkt Ndungulile alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Suzan Lyimo aliyeomba maelezo kutoka serikalini kuhusu matatizo ya kiafya yanayoweza kuwapata wanawake wanaokuza baadhi ya sehemu za miili yao.

Akijibu swali hilo Naibu Waziri alisema dawa na sindano zinazotumika kukuza maumbile ya miili ya wanawake ni hatari kwa sababu zinaharibu kinga ya mwili na hivyo kushindwa kupambana na magonjwa pamoja na mionzi.

“Serikali haijaruhusu utaratibu huu na ndio sababu tunapambana kuhakikisha kuwa haturuhusu kuingizwa nchini dawa ambazo hazitakiwi,” alisema Naibu Waziri.

Mbunge Suzan Lyimo aliuliza swali hilo baada ya kuwapo kwa idadi kubwa ya wanawake wanaotumia dawa mbalimbali kukuza maimbili yao, ndipo akataka kujua kama serikali inafahamu jambo hilo, na imechukua hatua gani.

Post a Comment

0 Comments