YANGA YAZIDI KUANDAMWA NA MAMBO MAGUMU NA MAZITO

Uongozi wa Yanga umethiitisha kuwa mlinda lango namba moja, Youthe Rostand hatakuwemo kwenye kikosi cha Yanga kitakachoivaa Njombe Mji kesho Jumanne, February 06.

Rostand aliumia kwenye mchezo dhidi ya Lipuli FC na alilazimika kubaki Iringa kwa matibabu zaidi asubuhi kabla ya kurejea Dar es Salaam jioni ya jana kwa usafiri wa ndege.

Wakati huo huo mlinda lango Benno Kakolanya amerejea kikosini baada ya kupona majeraha yake.

Kakolanya pamoja na Ramadhani Kabwili ndio wanaotegemewa kuibeba Yanga kwenye mchezo dhidi ya Njombe Mji pengine na ule wa ligi ya mabingwa dhidi ya St Louis Jumamosi ijayo.

Kuumia kwa Rostand kunaongeza Idadi ya majeruhi wa Yanga kufikia 11 idadi sawa na kikosi kamili kinachoweza kupambana uwanjani.

Wachezaji wa Yanga ambao ni majeruhi mpaka sasa ni:
1.Youthe Rostand
2.Juma Abdul
3.Haji Mwinyi
4.Abdallah Shaibu
5.Andrew Vicent
6.Pato Ngonyani
7.Yohana Nkomola
8.Thaban Kamusoko
9.Hamis Tambwe
10.Donald Ngoma
11.Ibrahim Ajibu

Credit-nijuzehabari

Post a Comment

0 Comments