Uzinduzi huo umefanyika katika ibada takatifu iliyoongozwa na Askofu wa kwanza wa Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria Daktari Emmanuel Joseph Makala
Katika risala yake mwenyekiti wa kamati ya kikosi kazi Bwana Shuma amesema mchakato wa kuanzisha shule hii ulianzishwa mwaka 2015 chini ya mchungaji Helman Gacha aliyeleta wazo la kuanzisha kituo Day Care center na wazo hilo lilipokelewa na kuanza kutekelezwa mara moja.
Baadae usharika uliamua kununua kiwanja kwa ajili ya kuendeleza shule hiyo na kiwanja hicho kilipatikana maeneo ya Lubaga manispaa ya Shinyanga. Chini ya mchungaji Harlod Mkalo pamoja na mchungaji mwenza Mathias Masele waliamua kuongeza nguvu kazi ndani ya kamati ya kikosi kazi ili kuhakikisha mambo hayakwami
Mwenyekiti wa kamati hiyo alisema wakati shule hiyo inaanzishwa rasmi ilianza ikiwa na wanafunzi wawili na walimu wawili na baada ya miezi mitatu idadi ya wanafunzi ilifikia 27.
Askofu Dr Emmanuel Joseph Makala,wakuu wa majimbo pamoja na wachungaji wakiendelea na ibada ya uzinduzi wa shule
Askofu Dr Emmanuel Joseph Makala akijiandaa na ufunguzi
Baada ya uzinduzi na uwekaji wakfu wa Shule ya Makedonia English medium
Askofu Dr Emmanuel Joseph Makala akiendelea na ufunguaji wa majengo ya shule hiyo












0 Comments