IFAHAMU SABABU ILIYOMFANYA PABLO AKATAE KUPOKEA BARUA YA KUVUNJA MKATABA NA SIMBA....YEYE MWENYEWE AFUNGUKA


Jana klabu ya Simba sc iliamua kuachana na kocha aliyekuwa anainoa timu hiyo Pablo Franco Martine baada ya kushindwa kutimiza matakwa ya mkataba wake. Awali baada ya uongozi wa simba kumwandikia barua ya kuvunja mkataba, Pablo alikataa kuipokea barua ile kwa kuwa ilikuwa na mapungufu.


"Ni kweli tulikuwa na kikao na mabosi wangu na kuna mambo sikukubaliana nayo hususani upande wa usajili, jioni CEO alinitumia barua ya kuvunja mkataba lakini ilikuwa na upungufu hivyo sikusaini nilimrudishia ili arekebishe.

"Sikupanga kuondoka Simba kwani tayari nilikuwa nimeikatia Visa familia yangu ya kuishi hapa kwa mwaka mmoja, hivyo nasubiri akirekebisha hiyo barua na kuyaweka yale niliyoyapendekeza ambayo ni maslahi basi nitasaini kuvunja mkataba," amesema Pablo ambaye aliingia Simba Novemba mwaka jana.

Post a Comment

0 Comments