Maajabu! TWIGA WASIMAMISHA BASI NA KUANZA KUKAGUA MIZIGO YA ABIRIA

Abiria waliokuwa wakisafiri kwenda sehemu mbalimbali Kaunti ya Laikipia walikumbwa na tukio barabarani lililowashangaza na hata kukatiza safari zao kwa muda. 

Twiga wa Laikipia wanadaiwa kuwa na tabia kama ya mbwa wa askari na kwa urefu wao hukagua na kuchukua mizigo ya abiria juu ya gari. Tukio hilo lilitokea wakati twiga alipochomoza kutoka vichakani na kusimama katikati mwa barabara na kulazimisha dereva kusimamisha gari na kumpa nafasi kufanya alichotaka. 

Abiria nao walipata fursa ya kumwangalia na kujionea twiga huyo ambaye hakuwa na haraka ya kumaliza shughuli zake. Tukio hilo ‎lilitokea kilomita 35 kutoka Rumuruti, mjini Laikipia kuelekea Kaunti ya Samburu. Kulingana na Kennedy Livingston, twiga wa eneo hilo ambalo lina vivutio kadhaa vya watalii ikiwa ni pamoja na wanyamapori, wana tabia hiyo na kwa urefu wao hukagua na kuchukura mizigo ya abiria mfano wa mbwa wa polisi. 

Tukio hilo limewaacha wengi na mshangao mkubwa, kwani kuna waliokuwa wakisafiri na ambao maishani mwao hii ilikuwa mara yao ya kwanza kumwona mnyama huyo wa porini hasa wasiokuwa wenyeji. Twiga kutafuta chakula Katika picha zingine ambazo tumeziangaia kwa makini, huenda wanyama hao hutafuta chakula na maji kwenye mizigo ya abiria kwani mara kwa mara hutokea wakati basi linaposimama na labda abiria akitaka kushuka.

Tofauti na wanyama wengine wakali wanaoishi porini, twiga ni mmoja wa wanyama ambao hupenda kutangamana na binadamu bila ya kuhisi maisha yake kuwa hatarini. 

Pia ni miongoni mwa wanyama ambao hawasumbuani na binadamu hasa katika kuharibu mimea mashambani kama vile ndovu, kiboko na hata mbogo. Hata hivyo waliomwona mnyama huyo walifurahia utalii wa ndani na bure.

Chanzo - Tuko

Post a Comment

0 Comments