Rais Samia: MAFUTA NI JANGA LA ULIMWENGU, SI LA SERIKALI YAMEPANDA DUNIANI KOTE

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Wananchi wa Kata ya Bwanga Wilaya ya Chato Mkoani Geita alipokua njiani akielekea Mkoani Kagera kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu inayoanza tarehe 08 Juni, 2022.

RAIS Samia Suluhu Hassan leo Jumatano Juni 8, 2022 amezungumza na Wananchi wa Bwanga Wilayani Chato, Mkoani Geita amesema kwasababu ya Vita inayoendelea Nchini Ukraine, bei ya mafuta imepanda duniani kote

Amesema “Bilioni 100 zimetolewa kufidia bei za mafuta zishuke. Mwezi huu bei zimeanza kushuka polepole. Tutaendelea kutoa Ruzuku mpaka duniani kukae sawa. Tutakata Bilioni 100 kila mwezi kwenye matumizi ya Serikali ili kupunguza makali”

Ameongeza “Dunia nzima tunaziambia zile Nchi mbili ziache kupigana kwasababu zikiacha, tutapata unafuu wa mambo mengi. Tulikuwa tunaagiza ngano katika mojawapo ya Nchi zinazopigana, sasa haiwezekani. Nchi nyingine mikate ni kwa mgao”

Post a Comment

0 Comments