SPIKA WA BUNGE TULIA ACKSON ATOA SIKU TANO KWA WAITARA NA MULUGO KULETA USHAHIDI BUNGENI KUHUSU MAUAJI

Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson ametoa siku tano kwa Mbunge wa Tarime Vijijini, Mwita Waitara na Mbunge wa Songwe, Philip Mulugo kuwasilisha kwake ushahidi wa tuhuma walizozitoa bungeni leo Ijumaa June 3, 2022 za mauaji yanayotokana na wanyama na walinzi wa hifadhi za misitu.

Agizo la Spika limetokana na michango ya wabunge hao kwa nyakati tofauti kwenye Wizara ya Malisili na Utalii ambapo wamedai kuwa wananchi wa majimbo yao wauawa na wanyama.

Wabunge hao pia wameliambia Bunge kuwa Kamati ya Mawaziri nane haijawahi kusaidia kitu chochote katika migogoro hiyo licha ya kueleza kuwa kamati hiyo ilifika katika mikoa yote ila wamedai katika mikoa yao hawajawahi kufika kumaliza migogoro hiyo.

Mbunge Waitara ametaja majina ya 14 ya watu katika jimbo lake ambao amedai kuwa waliuawa ama kupotea akiwatuhumu wahifadhi katika hifadhi ya Serengeti kwamba wamekuwa chanzo cha matukio hayo.

Mbunge huyo amesema hakuna maelewano baina ya wananchi na watu wa hifadhi kutokana na kukithiri kwa migogoro baina yao.

Kwa upande wake Mbunge wa Songwe, Philip Mulugo amedai watu 80 wameuawa kwa kuliwa na wanyama na wengine kujeruhiwa na kubaki na ulemavu wa kudumu.


Mulugo amesema amekusanya ushahidi wa kutosha kutoka katika halamshauri yake pamoja na wananchi.

Post a Comment

0 Comments