Wakazi wanaoshi katika hifadhi ya Ngorongoro ambao wameamua kuhama kwa hiari kwenye eneo hilo na kwenda kuishi Msomra Wilaya ya Handeni Mkaoni Tanga, wamemshukuru Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na Serikali kwa kuweka mazingira na utaratibu mzuri wa kuwahamisha wao pamoja na mali zao kufika katika makazi mapya.
Wakazi hao wametoa shukrani za juzi Jumatano Juni 15, 2022 wakati wakiendelea na zoezi la kupakia mizigo na mali zao kwa ajili ya safari ya kwenda Msomera, Handeni mkoa wa Tanga.
“Tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa sababu ameonesha kutujali sana kwani Serikali imetulipa fidia lakini mama kwa huruma yake akatuongezea hivyo tumefarijika na tunaondoka tukiwa na amani kubwa moyoni na tunamuombea kwa Mungu Rais wetu na Serikali yake waendelee kufanya kazi na kutuletea maendeleo sisi wananchi”, ameeleza Mzee Samuel Dadiel Huho (60) kutoka Kijiji cha Kimba kilichopo eneo la Hifadhi ya Ngorongoro.
“Maisha ya hapa hayana uhakika na ukitaka kujenga mpaka kibali tena kwa masharti, sasa hayo ni maisha gani? ninatoka eneo duni kwenda eneo bora zaidi. Kule nina nyumba nzuri niliyojengewa na Serikali, shamba la kulima na kuna huduma zote za kijamii, nawashukuru Viongozi wa Serikali kuanzia Mheshimiwa Rasi Samia, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu na Watendaji wote kwa kututhamini sisi tulioamua kuondoka kwa hiyari. Kuondoka kwetu ni faida kwa Taifa maana mazingira ya hifadhi yatalindwa na kuleta manufaa kwa
Taifa”, anaeleza Olemokolo ambaye ana mke na Watoto wawili.
Jumla ya familia 27 kati ya 103 zilizoamua kuondoka kwa hiyari eneo la Hifadhi la Ngorongoro zinasafirishwa na Serikali katika awamu ya kwanza kuelekea Msomera, Wilaya ya Handeni Mkoa wa Tanga kwa ajili ya kuanza makazi mapya ili kupisha uhifadhi katika eneo la Ngorongoro. Zoezi la kuwasafirisha wakazi waliosalia litaendelea katika awamu zingine ambapo Serikali itaendelea kuratibu kuhakikisha wanasafirishwa pamoja na mali zao
Chanzo - Channel ten
0 Comments