AZIZ KI AZUA JAMBO MITANDAONI, NI BAADA YA KUONEKANA AMEPIGA PICHA NA RAIS HERSI WAKIWA MAZOEZINI


Siku chache baada ya kukamilika kwa usajili wa kiungo Mshambuliaji Aziz Ki, wachambuzi wa michongo nchini Tanzania wameibuka na lawama nyingi baada ya kuonekana mchezaji huyo amepiga picha na Rais wa klabu hiyo ya yanga.

Wachambuzi wameibuka na hoja ya kwamba kwa mtu mkubwa wa klabu hiyo kuonekana amepiga picha na mchezaji mpya ndani ya klabu wakidai kuwa hiyo hali inaonesha upendeleo flani kwa mchezaji huyo na kudai anaweza kusababisha kuwagawa wachezaji hao.

Ikumbukwe tu kuwa Eng. Hersi Said ambaye ni Rais wa klabu hiyo kubwa hapa nchini amekuwa na utaratibu huo kwa muda wa siku nyingi, anashiriki mazoezi pale anapokuwa na nafasi ikiwa ni pamoja na kupiga picha na wachezaji wote.

Hapa chini nimekuwekea baadhi ya hizo picha;





Post a Comment

0 Comments