HAJI MANARA ATAJA SABABU ZA KUMTAMBULISHA AZIZ KI SAA 9:10 USIKU


Usiku wa kuamkia Leo Klabu ya Yanga iliwafanya wananchi na wadau wa soka nchini na nje ya nchi wakeshe wakisubiri utambulisho wa kiungo mshambuliaji Aziz Ki.

Nyota huyo akatambulishwa saa tisa na dakika kumi usiku na kukata kiu ya wananchi waliokuwa wakisubiri utambulisho wake kwa hamu.

Msemaji wa Yanga Haji Manara amesema lengo la klabu kufanya utambulisho wa Aziz Ki usiku wa manane ilikuwa kuonesha ukubwa wao tu.

Manara amesema walitaka kuionesha dunia kuwa Yanga inaweza kuugeuza usiku ukawa mchana.

Takwimu zimedhihirisha kauli ya Manara kwani baada ya Yanga kumtangaza Aziz Ki, ndani ya nusu saa wafuasi zaidi ya 10,000 walishiriki kutoa maoni katika post hiyo.

"Kiukweli hatukuwa na sababu yoyote zaidi ya kuonesha ukubwa wa Yanga, tulitaka tuwaambie watu kuwa Yanga inaweza kuufanya usiku mkubwa uwe na pilikapilika kama za mchana au jioni huku Instagram.

"Labda kuweka Tisa na dakika kumi ina maana tofauti kama picha inavyojieleza hapo juu. Ndio najua wapo waliotudhihaki na kusema tunaiua mitandao yetu wenyewe"

"Kwa jana ndio tukaambiwa hatufikiri sawa sawa. Wengine walienda mbali zaidi kwa kutukejeli kwamba tutapa likes na comments chache mno. Labda sasa watatupa heshima baada ya hizi takwimu za hapo chini."

"Mabibi na mabwana, saa tisa usiku, tena ndani ya nusu saa kupata comments zaidi ya elfu kumi sio jambo dogo. Hakuna club yoyote Afrika, inaweza kupata comments kama hizo ndani ya muda huo kwa utambulisho wa mchezaji tu, haipo klabu hiyo na kama ipo ntajiwe hapa."

"Tisa usiku upate comments elfu kumi kwa nusu saa? Ni yanga Afrikaaaaaaa. Na kuna wenzetu toka majuzi wana comments elfu sita kwa mchezaji tuliyeambiwa atatingisha dunia!"

"Aziiz Ki keshakusanya Comments 25 Elfu na ushee kwa masaa tu, ndugu zangu wao waliweka mchana kweupeeee, wanaume tumekandamiza Tisa Usiku, kisha tushawazidi kwa mbaaaali," alitamba Haji Manara

Post a Comment

0 Comments