HAYA HAPA MASWALI AMBAYO YANAWEZA KUULIZWA KWENYE USAILI WA SENSA 2022




Katia makala hii tumekuwekea maswali na yanayoweza kuulizwa katika usaili wa kuchambua watakaofuzu kwajili ya kufanya kazi za muda zilizotangzwa za sensa 2022

Sensa ni zoezi la ukusanyaji wa taarifa za watu na makazi yao, huweza kujumuisha aina ya makazi, kiwango Cha elimu, umri, kazi miongoni mwa taarifa nyinginezo ambazo hutakiwa kutolewa kwa usahihi. Zoezi la sensa linatarajiwa kufanyika Agosti 23 baadaye mwezi ujao.

1. Nini maana ya sensa

2. SENSA hufanyika kila baada ya miaka mingapi

3. Taja faida tano za sensa

4. Taja majukumu 5 ya karani wa sensa

5. Taja majukumu ya msimamizi wa sensa

6. Taja majukumu ya afisa Tehama katika sensa

7. Taja vifaa vinavyoweza kutumika katika zoezi zima la sensa

8. Taja taarifa zinazokusanywa katika zoezi la sensa

9. Taja sifa za mtumishi wa Uma

10. Kwanini taarifa za mtu binafsi zinapaswa kutunzwa kwa Siri?

11. Sensa inahusiana vipi na maendeleo?

12. Kuna tofauti gani ya sensa na ukusanyaji wa taarifa za anwani za makazi

13. Je ni mtu gani anayepaswa kuhesabiwa katika zoezi la sensa

14. Utafanyaje endapo hutapewa taarifa wakati wa zoezi la sensa

15. Kwanini nilazima kila mtu kuhesabiwa?

16. Data za sensa hutumika vipi kutathmini maendeleo

17. Nini maana ya Kaya?

18. Taja idadi ya mitaa katika katika kata yako

19. Taja kirefu Cha. nbs

20. Taja kauli mbiu ya sensa ya mwaka huu.

21. Nini maana ya mtaa

22. Maana ya kata

Nivyema kupitia vipengele mbalimbali ili uweze kuwa mahiri katika eneo hili. Aidha maswali haya yanatarajiwa kukupa mwanga wa Nini chakufanya ili uweze Kushinda usaili.

Post a Comment

0 Comments