MBWA AWALEA BATA 15 YATIMA BAADA YA MAMA YAO KUTOWEKA

Mbwa mwenye upendo amechukua jukumu la kuwalea bata mayatima 15 baada ya mama yao kutoweka ghafla.

Lakini Fred mwenye umri wa miaka 15, sio mgeni kuwa baba mlezi, mnamo 2018, aligonga vichwa vya habari alipolea bata tisa waliotelekezwa katika hali kama hiyo.

Miaka kadhaa baadaye, mbwa huyo mzee anajivunia kuwa baba wa kizazi kingine kipya.

Msururu wa picha zilizoonwa na Mirror zinaonyesha vifaranga wadogo wakiwa wamejikunyata katikati ya miguu ya mbele ya Fred na kupumzika wakiwa wamelala pamoja kwenye jua.

Vifaranga hao wenye rangi ya manjano angavu wanaonekana kuwa na furaha na starehe wakiwa karibu na mzazi wao mpya.

Tangu mama yao kutoweka kwa njia isiyo ya kawaida, Fred amehakikisha kuwa anawatunza watoto wake wapya akiwabeba mgongoni mwake na kuwaonyesha wafanyakazi na wageni.


Mmiliki wa mbwa huyo alisema hashangazwi kwamba Fred alipata familia mpya.

"Kwa muda wa miaka 15 ya kummiliki, Fred ametumia muda mwingi katika Kasri hilo na wanyama hao na imekuwa tabia ya pili kwake kuwa miongoni mwa wanyama mbalimbali waliookolewa," alieleza.
Mbwa atunza watoto wachanga waliotelekezwa shambani

Katika makala tofauti, mtoto mchanga aliyetelekezwa shambani alinusurika usiku wa baridi kwa hisani ya mbwa na watoto wa mbwa.

Daily Mail inaripoti kuwa mtoto huyo wa kike aliachwa usiku bila nguo katika jimbo la Chhattisgarh nchini India.

Mtoto huyo alipatikana siku iliyofuata saa 11 alfajiri akiwa amejilaza karibu na mbwa na watoto wa mbwa ambao walimpa joto.

Alipatikana bila majeraha baada ya kusikika akilia na wenyeji. Picha za ajabu zilionyesha mtoto huyo akiwa amekaa pamoja na watoto wa mbwa kwenye majani.

Mmoja wa wenyeji ambaye hakutaka jina lake litajwe alisema kuna uwezekano mbwa huyo aliokoa maisha ya mtoto huyo.

Post a Comment

0 Comments