Rasmi: AZIZ KI NI MWANANCHI


KLABU ya Yanga SC imetangaza kukamilisha usajili wa kiungo Mshambuliaji Stephane Aziz Ki raia wa Burkina Faso mwenye umri wa miaka 26 kutoka ASEC Mimosas ya Ivory Coast kwa mkataba wa miaka miwili.

Usajili wa Aziz Ki unakuwa usajili mpya wa tano (5) wa Yanga SC baada ya beki Mcongo, Lomalisa Mutambala kutoka Sagrada Esperança ya Angola

Wengine ni kiungo Mrundi, Gael Bigiriamana kutoka Glentoran ya Ireland Kaskazini, winga Mghana, Bernard Morrison kutoka Simba SC na mshambuliaji Lazarous Kambole kutoka Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini.






Post a Comment

0 Comments