SIMBA SC YAWEKA WAZI SABABU ZA KUWEKA KAMBI NCHINI MISRI

Afisa Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Simba

Afisa Mtendaji mkuu wa klabu ya Simba Barbra Gonzalez ameweka wazi sababu za klabu ya Simba kuweka kambi nchini Misri.

Akizungumza na waandishi wa habari Ijumaa ya leo Barbra amesema klabu hiyo wameweka kambi nchini Misri ili kuipa nafasi timu hiyo kukutana na timu nyingi nzuri ambazo zitawapa changamoto ya kujifahamu wako kiwango gani.

Barbra amesema timu kubwa kama Al Ahly wamejaribu kuongea nao ili waweze kupata mechi ya kirafiki na timu hiyo ila inaonekana ni ngumu kwa timu hiyo kufanikiwa hilo kutokana na ligi kuu ya nchini Misri bado inaendelea na Al Ahly bado wanakabiliwa na mechi 13 hadi ligi itakapoisha

Post a Comment

0 Comments