YANGA YAMALIZANA NA CHICO USHINDI



UONGOZI wa klabu ya Yanga umetangaza rasmi kuachana na winga Chico Ushindi ambaye amemaliza mkataba na timu hiyo ili kubaki na mastaa 12 wa kigeni.

Wakati huo huo kwa upande wa wachezaji wa ndani Yanga imeachana na Balama Mapinduzi, Deus Kaseke, Yassin Mustafa na Paul Godfrey

Msemaji wa Yanga, Manara amesema wanajumla ya wachezaji 14 wa kigeni hadi sasa kwa mujibu wa sheria wanatakiwa wachezaji 12 ndio sababu iliyowafanya wampunguze staa huyo.

"Tunaachana na Ushindi ambaye tuliingia naye makubaliano maalum akitokea TP Mazembe na tutafanya mazungumzo na Yacouba ambaye hayupo fiti kutokana na kutoka kukaa nje ya uwanja kwa muda mrefu kutokana na kusumbuliwa na majeruhi," alisema.

Kuondoka kwa mastaa hao Yanga itakuwa na wachezaji Djigui Diarra, Djuma Shaban, Yanick Bangala, Khalid Aucho, Jesus Moloko, Fiston Mayele, Heritier Makambo, Stephane Aziz Ki, Bernard Morrison, Gael Bigirimana, Joyce Lomalisa na Lazarous Kambole.

Post a Comment

0 Comments