Askofu wa KKKT- DKMZV Daktari Emmanuel Joseph Makala
Na
NEEMA ENOCK - SHINYANGA:
Askofu wa kanisa la Kiinjili La Kilutheri Tanzania Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria (Shinyanga& Simiyu), Daktari Emmanuel Joseph Makala amewataka wachungaji na watumishi wa Mungu kuishi maisha ya unyenyekevu na kujitoa kwa ajili ya wengine kama Kristo alivyojitoa ili waweze kuzaa matunda ya pendo lake na kuujenga ufalme wa mbinguni.
Askofu Makala ameyasema hayo wakati wa ibada ya kustaafu kwa Mchungaji Daniel Msengi ibada iliyofanyika Jumapili ya tarehe 21 Agosti, 2022 katika Kanisa la KKKT Usharika wa Shagihilu Jimbo la Kishapu Shinyanga.
Pia Makala amempongeza Mchungaji Daniel Msengi kwa kujitoa kwa moyo kuifanya huduma ya Mungu katika mazingira yote kwa takribani zaidi ya miaka 38 pasipo kusukumwa wala kulazimishwa.
Pia ibada hiyo imehudhuriwa na Msaidizi wa Askofu wa Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria Dkt Yohana Nzelu, Katibu Mkuu wa Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria Bi. Happnes Gefi, wakuu wa majimbo wa Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria Wachungaji, wadiakonia na Wakristo kutoka sharika mbalimbali zilizopo ndani na nje ya Dayosisi hiyo
Askofu Makala akiendesha ibada ya kumstaafisha mchungaji Daniel MsengiAskofu Makala akitoa baraka kwa Mchungaji Daniel Msengi pamoja na mke wake wakati wa ibada ya kustaafu kwake
Msaidizi wa askofu ya Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria Daktari Yohana Nzelu wakati wa ibada ya kustaafu kwa Mchungaji Daniel Msengi
Katibu mkuu wa Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria Bi. Happiness Geffi akitambulisha wageni wakati wa ibada ya kustaafu kwa Mchungaji Daniel MsengiAskofu Makala akiwa na baadhi ya wachungaji wa KKKT- DKMZV mara baada ya ibada ya kustaafu kwa Mchungaji Daniel Msengi
Wachungaji wa Kilutheri walioshiriki ibada ya kustaafu kwa Mchungaji Daniel MsengiWakristo wakifuatilia matukio katika ibada ya kustaafu kwa Mchungaji Daniel Msengi
Wakristo wakifuatilia matukio katika ibada ya kustaafu kwa Mchungaji Daniel Msengi
0 Comments