BAADA YA MECHI YA NGAO YA HISANI, HII HAPA TAREHE YA SIMBA NA YANGA KUKUTANA TENA


WATANI wa jadi Yanga na Simba zitakutana katika mchezo wao wa kwanza wa Ligi Kuu ya soka Tanzania bara msimu wa 2022/2023 Oktoba 23 uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa ratiba ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania(TPLB) katika mchezo huo namba 64 wa raundi ya 8 Yanga itakuwa mwenyeji.

Mchezo wa Ngao ya Jamii wa ufunguzi wa Ligi Kuu kati ya Yanga na Simba umepangwa kufanyika Agosti 13 huku ligi ikianza Agosti 15.

Ihefu iliyorejea ligi kuu itakuwa mwenyeji wa Ruvu Shooting wakati Mtibwa Sugar itakuwa wageni wa Namungo.

Post a Comment

0 Comments