MREMA ALIKUWA MTANZANIA PEKEE ALIYEWAHI KUWA MBUNGE WA MAJIMBO MATATU TOFAUTI KWA VYAMA VYA SIASA VITATU TOFAUTI



Taifa la Tanzania likiwa katika wakati wa kuomboleza kifo cha mwanasiasa Augustino Lyatonga Mrema aliyewahi kuleta upinzani mkubwa wa kisiasa katika siasa za Tanzania aliyefariki tarehe 21 Agosti, 2022 MASENGWA BLOG inaendelea kukuletea matukio muhimu yaliyowahi kutokea katika medani za siasa za mwanasiasa huyo.

Moja ya jambo ambalo linatajwa kuwa limewahi kutokea kwake tu, Augustino Mrema anatajwa kuwa mwanasiasa na mtanzania pekee aliyewahi kuwa mbunge katika majimbo matatu tofauti kupitia vyama vitatu tofauti.

Kwanza, Mrema amewahi kuwa mbunge wa jimbo Moshi vijijini kati ya mwaka 1980 hadi 1995 kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)

Pili, amewahi kuwa mbunge wa jimbo la Temeke lililopo Jijini Dar es Salaam kati ya mwaka 1996 hadi 1998 kupitia chama cha NCCR-MAGEUZI

Tatu, Kati ya mwaka 2010 hadi 2015, Augustino Lyatonga Mrema amewahi kuwa mbunge wa jimbo la Vunjo lilipo mkoa wa Kilimanjaro kupitia chama cha Tanzania Labour Party (TLP)1.1980 - 1995 MOSHI VIJIJINI (CCM), 2. 1996 - 1998 TEMEKE (NCCR- MAGEUZI), 3. 2010 - 2015 VUNJO (TLP).

Marehemu Lyatonga Mrema pia atakumbukwa kwa kuanzisha ulinzi shirikishi Tanzania (Sungusungu)

Post a Comment

0 Comments