WALIOOBEZA USAJILI WA MORRISON YANGA WAANZE KUHESABU TAKWIMU ZAKE

Jana winga Bernard Morrison alitoa assist yake ya kwanza ya Ligi kuu ya NBC akimtengenezea Bakari Nondo Mwamnyeto kufunga bao la ushindi la Yanga kwenye dakika ya 85 katika mchezo ambao yanga iliibuka na ushindi wa mabao 2-1

Morrison aangewezakuondoka na bao pia kama shuti lake lililogonga mamba wa juu na kuvuka mstari lingekubaliwa.

Wakati Yanga ilipomrejesha Morrison kutoka simba wapo walioponda usajili huo wakidai hakuwa na takwimu nzuri katika misimu miwili aliyoitumikia Simba

Lakini wakisahau takwimu nzuri alizoondoka nazo Yanga alipokwenda kujiunga Simba

Morrison karudi jikoni ambako chakula kinapikwa, muhimu wahesabu tu takwimu zake, tayari ana assist moja

Post a Comment

0 Comments