
Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama na Mkuu wa wilaya ya Rombo, Agnes Hokororo alisema ajali hiyo ilihusisha magari mawili pamoja na pikipiki moja.
Wengine waliofariki katika ajali hiyo ni pamoja na Anastazia Malaysia ambaye ni Mwenyekiti wa UWT Tawi la Chuo Kikuu Cha Ushirika Moshi (Mocu) na mkazi wa Shimbi, Rombo, na Edwin Msele, katibu wa hamasa Shirikisho la vyuo vikuu Moshi mjini.
Wengine ni Ally Mbaga (Mjumbe wa NEC) wilaya ya Same na mkazi wa Mwanga, mwanamke ambaye jina halijatambulika aliyekuwa kwenye gari la Fuso, mkazi wa Himo, mwanamke aliyekuwa kwenye bodaboda ambaye fuso liligonga pikipiki hiyo na mtu mwingine mmoja ambaye hajafahamika.
Hokororo amesema majeruhi ni mwanahabari Jackson Kimambo aliyekuwa dereva wa Toyota surf hali yake inaendelea vizuri akipata matibabu hospitali ya rufaa ya KCMC.
Miili ya marehemu wote imehifadhiwa chumba cha kuhifadhi maiti katika hospitali hiyo.
Taarifa za awali kutoka eneo la tukio zinaeleza chanzo cha ajali hiyo ni kuwa gari la Fuso lilifeli breki na kugonga gari hilo kwa nyuma kabla ya kuiparamia na kuigonga pikipiki na kusababisha vifo hivyo.
Anord Swai enzi za uhai wake
Marehemu Anord Swai enzi za uhai wake

