HIVI NDIVYO IBADA YA JUMAPILI MARCH 05, 2017 ILIVYOENDESHWA KATIKA KANISA LA KKKT USHARIKA WA EBENEEZER KANISA KUU SHINYANGA




Mchungaji Jackson Maganga akihubiri.
Ibada iliyofanyika katika Kanisa la KKKT usharika wa Ebeneezer Kanisa Kuu Shinyanga siku ya Jumapili ya tarehe 05/03/2017  ilikuwa ibada iliyoja baraka nyingi na utukufu

Kichwa cha somo cha siku cha siku hiyo kilikuwa;
TUKIMTEGEMEA MUNGU TUTASHINDA MAJARIBU

"Basi mfalme akaenda Gibeoni, ili atoe dhabihu huko, kwa kuwa ndipo mahali pa juu palipo pakuu. Sulemani akatoa sadaka elfu za kuteketezwa juu ya madhabahu ile. Na huko Gibeoni BWANA akamtokea Sulemani katika ndoto ya usiku, Mungu akamwambia omba utakalo nikuone. Sulemani akasema, umemfanyia mtumwa wako Daudi baba yangu fadhili kuu, kadri alivyoenenda mbele zako katika kweli, na katika haki, na katika unyoofu wa moyo pamoja nawe, nawe umemwekea na fadhili hii kuu, maana umempa mwana wa kuketi kitini pake kama ilivyo leo.

Na sasa, Ee BWANA Mungu wangu, umenitawaza niwe mfalme mimi mtumwa wako ,badala ya Daudi baba yangu; nami ni mtoto mdogo tu; sijui jinsi inipasavyo kutoka wala kuingia. Na mtumwa wako yu katikati ya watu wako uliowachagua; watu wengi wasioweza kuhesabiwa, wala kufahamiwa idadi yao, kwa kuwa ni wengi. Kwa hiyo nipe mimi moyo wako wa adili niwahukumu watu wako, na kupambanua mema na mabaya; maana ni nani awezaye kuwahukumu hawa watu wako walio wengi?

Neno hili likawa jema machoni pa Bwana, ya kuwa Sulemani ameomba neno hili. Mungu akawaambia, Kwa kuwa umeomba neno hili, wala hakujitakia maisha ya siku nyingi; wala hukutaka utajiri kwa nafsi yako; wala hukutaka roho za adui zako; bali umejitakia akili za kujua kuhukumu;'' 1Wafalme 3:4-11

Akiwa anahubiri mchungaji Jackson Maganga alisema kuwa
''Katika kitabu hiki tunaona kuwa kulikuwa na ushindani mkubwa kati ya Daudi na watu wake hasa ni nani awe mfalme baada ya yeye.''

''Hii ilikuja baada ya mfalme Daudi kuzeeka na akahitajika mfalme mwingine atakayerithi kiti cha Daudi.

Tunamuona Adonia kaka yake na Sulemani akiitaka hii nafasi ya ufalme kwa nguvu nyingi.''

''Adonia anaamua kusimama na kujitangaza mfalme mbele ya watu wake. Tunamuona anaandaa karamu na kuchinja vinono.''

''Pamoja na hayo, Bwana anasema kuna mtu mwingine ambaye atakuwa mfalme tofauti na Adonia ingawaje kuna mwingine anayejitangazia ufalme.''

''Katika kipindi hiki Sulemani alijikuta akiwa na wakati mgumu sana uliomfanya afadhaike na kuhuzunika sana kwa maana alijua Adonia akiwa mfalme hakika Adonia atamuua Sulemani. Akili ya Sulemani ilivurugika sana maana ndugu yake alikuwa anaenda kutoa uhai wake''

''Pamoja na yote hayo, Sulemani hakusema neno lolote wala hakutenda jambo lolote zaidi ya kumwangalia Bwana''

''Daudi akaagiza wamtoe Sulemani wamtembeze katika njia zote na kumthibitisha kuwa ni mfalme.''

''Ndivyo ilivyo hata sasa kwako mkristo wa leo maana una vita iliyopo kwako. Watu watakupiga vita sana na watakusema sana. Lakini jua kuwa Mungu ana makusudi na wewe, ana makusudi na maisha yako, hivyo usiogope vitisho vya maadui.''

''Najua unakutana na mambo magumu yanayovunja moyo, yanayokufadhaisha na kukuhuzunisha. Endelea kusimama na kumtegemea Mungu aliye hai kwani najua Mungu amekuokoa mambo mengi magumu. Kwani ni mara ngapi Tunasimama mbele za Mungu kumshukuru? Siku zote tunasimama mbele zake kumshukuru kwa kuwa anatusaidia pale tunapokutana na magumu.''

''Unaposimama kumshukuru kutoa sadaka mbele za Mungu, Sadaka yako unayoitoa inakuwa itikio na inamlazimu Mungu kujifunua kwako. Hivyo endelea kusogea mbele za Mungu kumshukuru kwa sadaka ili aendelee kujifunua kwako kwani hata baada ya Sulemani kuthibitishwa alimtolea sadaka ya wanyama maelfu.''

''Katika sadaka hiyo Mungu aliendelea kujidhihirisha kwa Sulemani kwani alimtokea usiku na kumwambia aombe lolote atakalo. Kilichomshangaza Mungu ni pale alipoona Sulemani akiomba kupewa hekima. Mungu alimpa Sulemani hekima ambayo hapana mwanadamu aliyewahi kuipata.''

''Sadaka yako ikawe itikio kwa Mungu katika kujibu haja za moyo wako.''

''Bwana aendelee kusema na kila mmoja wetu akaweze kujifunua kwetu''

''Nawe mtegemee Mungu aliye hai ambaye anaweza kufanya kitu cha ziada zaidi''

''BWANA ALIBARIKI NENO LAKE LIKAFANYIKE KUWA MSAADA KATIKA MAISHA YETU, KWA JINA LA BABA NA LA MWANA NA LA ROHO MTAKATIFU

AMEEE !!''





Msaidizi wa Askofu na Dean wa Kanisa Kuu usharika wa Ebeneezer mchungaji Trafaina A. Nkya.

Katika ibada hiyo Dean aliwatambulisha wahasibu walioajiriwa na Dayosisi pamoja na usharika ambao nI Neema Benjamin na Vedasto Musoline Zimbeiya .


Mtunza hazina wa usharika NEEMA BENJAMIN, aliyetambulishwa kwa mara ya kwanza katika ibada mara baada tu ya kuajiriwa.


Vedasto Musoline Zimbeiya, mhasibu mpya wa jimbo ambaye hajapangiwa kituo cha kazi akitambulishwa mbele ya washarika.

Pia Dean wa kanisa Kuu alitoa salaamu mbalimbali kutoka makao makuu ya Kanisa KKKT Arusha ambako amekuwa huko kwa muda wa wiki mbili


Mwinjirist Elisha Swai akisoma matangazo ya usharika katika ibada ya leo

Pia alitoa salaam na taarifa fupi ya kwaya ya vijana ambayo tarehe 18/02/2017 ilisafiri kwenda wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro katika katika usharika wa NRONGA kwa ajili ya huduma ya uinjiristi. Katika ziara hiyo kwaya ya vijana walifika mnamo saa tatu na robo usiku siku ya Jumamosi na siku iliyofuata (JUMAPILI ya tarehe 19/02/2017) walihudumu katika ibada ya kwanza na ya pili na jioni kukafanyika semina ya neno la Mungu.

Siku ya zilizofuata kwaya ya vijana walifanya uinjiristi wa nyumba kwa nyumba katika mitaa yote ya usharika huo ambapo waliweza kuwafikia zaidi ya watu 250 ambapo waliweza kumuona Mungu kwa viwango visivyo vya kawaida kwani watu wengi waliokuwa wamekata tamaa walifunguliwa.

Pia walifanya udiakonia kwa kutembelea wagonjwa na wasiojiweza wapatao 30 kupitia misaada mbalimbali pamoja na neno la Mungu na maombi.

Pia waliendesha mafunzo kwa njia ya sinema na zaidi ya watu 35 walikata shauri la kumpokea Yesu kama Bwana na mwokozi wa maisha yao.

Kulingana na huduma iliyotolewa na kwaya ya vijana, ilipelekea kualikwa tena mnamo mwezi wa saba kwa huduma kama hiyo kwani ni watu wengi sana hawakufikiwa kulingana na muda kuwa mdogo.

Mnamo tarehe 24/02/2017, kwaya iliondoka katika usharika wa NRONGA kuelekea Moshi mjini ,ambapo waliwezakutembelea makao makuu ya Dayosisi ya Kaskazini pamoja na kujifunza miradi mbalimbali na baadae waliondoka kuelekea usharika wa Masame kati alikotoka mwinjiristi wa usharika wa Ebeneezer Kanisa Kuu Shinyanga Elisha Swai ambapo walipokelewa na viongozi wa idara pamoja na mchungaji wa usharika na baadae walielekea usharika wa Masama na kuanza mkutano wa injili.
Siku zilizofuata kwaya ilifanya uinjiristi wa nyumba kwa nyumba na kuweza kufanikiwa kutembelea zaidi ya kaya 160 kwa neno la Mungu na maombi . Mungu alizidi kujifunua kwa mambo makubwa kwani waliona nyoka wakitoka ndeni na kukimbia watu wakiacha vitu vyaovya kichawi na kurudi kwa Yesu, waliokata tamaa walitiwa nguvu, pia walishuhudia kuona mtu aliyekuwa katika hali ya kufa Mungu akimpa uhai na uzima tena baada ya maombi yaliyoongozwa na msaidizi wa Askofu Trafaina Nkya na mchungaji kiongozi wa usharika huo pamoja na kikundi cha wanamaombi.


Katika huduma hiyo pia walikutana na mtu ambaye amekaa muda wa miaka 10 bila kwenda kanisani kwa kukata tamaa lakini mara baada ya kuombewa na kutiwa nguvu siku ya Jumapili alikuwa wa kwanza kufika kanisani.


Hizi ni baadhi tu ya huduma kati ya nyingi walizozifanya kwaya ya Vijana walipokuwa katika ziara yao.


Walirudi Shinyanga tarehe 28/02/2017 wakifika nyumbani wakiwa salama. AMEEEN.

Msaidizi wa Askofu na Dean wa kanisa kuu Ebeneezer Trafaina A. Nkya ( kulia) na msaidizi wake Mchungaji Jackson Maganga wakiwa madhabahuni pa Bwana.

Mwimbaji wa nyimbo za injili Siza Mwapamba kutoka Dar es salaam akiwa anaimba katika ibada hiyo


Waimbaji wa kikundi cha kusifu na kuabudu wakimwabudu Mungu katika ibada hiyo.


Katibu wa Usharika Ibrahimu A. Lyanga (kulia) akiwa ameketi pamoja na mwenyekiti wa kamati ya kushughulika maafa ya mtaa wa Konde Busongo


Washarika ibadani wakifuatilia ibada hiyo



Washarika wakiwa nje mnada ukiendelea


Washarika wakiwa nje mnada ukiendelea


Gerlad Mchau akipiga mnada vitu mbalimbali vilivyoletwa kwa ajili ya sadaka


Baada ya kutoka nje ibada inaelekea ukingoni kabisa

Baadhi ya washarika wakisalimiana na kupiga picha kwa pamoja mara baada ya ibada


MPIGA PICHA - ISAAC LUHENDE 
MASENGWA BLOG