
Amesema watu hao walijeruhiwa kwa kupigwa na mawe sehemu mbalimbali miili yao na wafanyabiashara wadogowadogo waliokuwa wakifanya biashara pembeni ya barabara wakishirikiana na watu wengine waliokua wakishabikia wakati wakiendelea na zoezi la kuwaondoa wafanya biashara wadogowadogo katika maeneo yasiyo ruhusiwa haswa kwenye hifadhi ya barabara ya mwanza kwenda shinyanga.
Aidh, Msangi amesema katika harakati za kudhibiti vurugu hizo askari walifanikiwa kuwakamata watu tisa ambao inadaiwa kuwa walikuwa wakihusika katika vurugu hizo kwa ajili ya mahojiano na uchunguzi utakapokamilika, watafikishwa mahakamani.
Majeruhi wote wapo hospitali ya mkoa ya Sekou Toure wakiendelea kupatiwa matibabu na hali zao inaendelea vizuri