JINSI RAISI MAGUFULI ALIVYOTUA DAR ES SALAAM AKITOKEA LINDI NA MTWARA

PICHA: Rais JPM alivyotua Dar leo March 05
MUUNGWANA BLOG / 7 hours ago
Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiongozana na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Hashim Mgandilwa mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea katika ziara ya kikazi katika mikoa ya Lindi na Mtwara jioni ya jana March 5, 2017.  
PICHA NA IKULU

Rais John Magufuli amewasili jijini hapa jioni ya jana  (Jumapili) baada ya kukamilisha ziara ya kikazi ya siku nne katika mikoa ya Pwani, Lindi na Mtwara.

Rais Magufuli amewasili  katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JKIA) akitokea Mtwara.  


Mara baada ya kuwasili, Rais Magufuli alipokelewa na viongozi mbalimbali akiwemo Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Hashimu Mgandilwa.

 Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Madawa ya kulevya nchini Bw. Rogers Sianga, mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea katika ziara ya kikazi katika mikoa ya Lindi na Mtwara jioni ya jana  March 5, 2017.

 Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) Mhandisi Ladislaus Matindi  mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea katika ziara ya kikazi katika mikoa ya Lindi na Mtwara jioni ya jana March 5, 2017