Kama hujawahi kuumizwa na mtu fulani, ukaumia ndani kabisa, inawezekana unatembea na hayo maumivu ndani ya mwili wako-hata kama ilitokea miaka iliopita
.muda huwa hauponyi vidonda vilivyopo,mpaka ushughulikie tatizo , tunatunza maumivu hayo ndani ya miili yetu. Tunajidanganya kwa kuvifunika vidonda tukijua kwamba tutapona kwa kuchagua mtu mwingine wa kukufanya uwe na furaha.
Unapovunjika moyo, waokoaji wetu hutuambia tufanye tuwezavyo ili kuachana na maumivu. Nilipojaribu kuondokana na huzuni ya ndani kutokana na kuumizwa mwanzo, afadhali ningejisikia kukimbia kabisa ili niondokane na maumivu.kwa sababu nilikuwa na nia ya kupona. Nilijua kukimbia haikuwa chaguo.
Katika majibu ya maumivu , wengi wetu hukimbia, wengine hujituliza, wengine hujirudisha wenyewe, na wengine hupatwa na hasira. Wengi wetu huumia kwa sababu huwa hatukubaliani na kilichotokea na kusamehe . jinsi wanavyokuwa na maumivu, uzoefu huu unaweza kutufundisha mambo mengi yanahusiana na maisha yetu- na kufanya utaratibu wa kusamehe.
Hapa kuna mambo machache ya kukumbuka katika safari yako ya kuachilia .
1.Jisamehe Mwenyewe, Sio Mtu Mwingine.
Kukataa kumsamehe mtu itakuumiza mwenyewe,na sio mtu mwingine. Uwezo wa kusamehe mara ngingi hutokana na shina lililoko ndani mwako la kuumiza mtu mwngine kama wewe ulivyouumizwa basi utataka kulipa kisasi, kumuumiza huyo tena. Inaweza pia ikawa ni woga wa kuachilia. Hatua ya kwanza ya kusamehe ni kujijali mwenyewe na kupata nafasi ya kujisamehe.
2.Kila Mtu Anajitahidi Kuwa Bora Kadri Awezavyo.
Haijalishi ni katika hali gani, mtu aliekuumiza hufanya awezavyo kuwa bora, wengi wetu huwa hawamuumizi mtu kwa makusudi , Inatokea’’. Kwa wale wanaokusudia, hufanya hivyo kwa sababu nao wameumizwa ndani ya mioyo yao. Kuendelea kurudi kwenye huu ukweli, msingi wake ni kusamehe. Inatusaidia kuona ubinadamu wa wale waliotuathiri badala ya kuanza kuwarudishia matendo mabaya. Nilipoumizwa na mtu fulani, sikubali na sikutaka kuongea , au kuwasema vibaya. Badala yake nilijaribu kuelewa kwa nini wameamua kufanya hivyo. Naamini kwamba wanafanya kwa sababu wanataka kupata kitu kilicho bora kwao na huenda kuna kitu wanakihitaji .
3.Ni wewe Pekee Unaweza Kujidhibiti.
Tunapokuwa tumeumizwa na mtu mara nyingi tunahisi hatuna nguvu. Tunapokubali huu ukweli, hurudisha lengo kwetu wenyewe. Mara zote kuna kitu tunachokidhibiti. Jifunze uwezacho kuhusiana na wewe mwenyewe na ukue. Chagua unataka uwe mtu wa aina gani badala ya kukazana na mambo yanayohusu watu wengine au hali iliopo ambayo huwezi kubadilisha.
4.Huanza Na Kujifunza Kutaka Vitu Vizuri Kwa Ajili Ya Watu Wengine.
Napenda kumtuma upendo na mwanga mtu alieniumiza .unaweza ukafikiria mtu aliesimama mbele yako , halafu moyo wako unaachilia upendo , na wao watakupa upendo pengine hata zaidi ya ulivyofanya. Ni zoezi zuri la kukusaidia kukumbuka kwamba upendo ni mzuri.kama ukitoa upendo , upendo huo utakurudia zaidi ya ulivyotoa. Upendo wako hauna kipimo.
5.Kuongelea Msamaha Wako Ni Muhimu.
Ninapohitaji kumsamehe mtu , huwa nasema hayo maneno kwa sauti mara moja iwezekanavyo. Huwa nawafikiria wao kuwa na furaha na amani ya kutosha , ambayo ni kitu ambacho kila mwanadamu anakihitaji maishani mwake. Mwanzo utakuwa unapata shida kama umeshikilia bila ya kuachilia msamaha. Lakini ukiachilia, utaanza kuona rahisi mwenyewe kusamehe, na maneno huja kwa urahisi kutoka mdomoni mwako, utaanza kuona mwanga na moyo wako utaanza kufunguka kwa kadri unavyoendelea kusema maneno hayo ya msamaha, na utaweza kuachia upendo kwa mtu aliekuumiza.
6.Upinzani Wa Kusamehe Huja Kutokana Na Kukataa Kutoa Maumivu.
Mara nyingi nitasema kwa sauti , nimekuachilia wewe,( unamtaja jina) ninapoanza kupata ufahamu kuhusu wao au hali ya maumivu, nitajiuliza ingawa kitu sio cha lazima.kuna sehemu ya afya ya uponyaji unapoondokana na maumivu, lakini hii inaweza ikawa ni majivuno pale mkanda unapoanza kucheza ndani yako kwa kurudia rudia yaliopita . jitahidi kuachilia yaliopita, na ukazanie yajayo unayotahili kuyapata.
7.Ni Mlolongo Mrefu.
Wakati mwingine maumivu huwa yamezidi sana kiasi kwamba huwezi kufikiria hata namna ya kusamehe. Ni muhimu kukumbuka kwamba msamaha una mpangilio wake. Kupona kuna njia zake. Tunafanya utaratibu. Tunafikiria tumesamehewa. Na mara tunakuwa ndani ya maumivu tena. Ni sawa katika kupitiia hali hizo, Anza utaratibu wa kusamehe kila kitu tena. Na uachilie .
Ingawa wakati mwingine tunaona kuwa ni vema kutoishi na maumivu , uzoefu huu ni mzuri, nafasi ya lazima kwenye maisha yetu tunapokua, tunapoamua kufanya mchakato