MZEE MAJUTO ATISHIWA KUUAWA

Siku 10 tangu muigizaji maarufu wa vichekesho Amri Athumani ali maarufu kama MZEE MAJUTO kutoa taarifa za kutapeliwa kwa milioni 25 na kampuni fulani kwa waziri wa habari na michezo mheshimiwa Harrison Mwakyembe.

Muigizaji huyo amefunguka na kudai kuwa kuna watu wasiojulikana wanaofuatilia maisha kwa kutaka kumuua

Ijumaa wikienda limeelezwa kuwa toka msanii huyo atoe malalamiko ya kutapeliwa kwa fedha zake hizo, amekuwa akiishi kwa maisha ya wasiwasi na mashaka zaidi huku akihisi kwamba kuna watu wanataka kumuua kwa sababu tu ya kudai haki yake

Post a Comment

0 Comments