MAMA DIAMOND AELEZA DIAMOND KUHUSISHWA NA MIMBA YA MOBETTO


Mama mzazi wa Diamond amesema kuwa taarifa hizo si za kweli kwa sababu yeye mkwe wake anayemjua ni Zari ambaye amemzalia wajukuu wawili.

“Umempa wewe? Hiyo mimba mimi siijui labda wewe, kwa sababu mimi sijui taarifa za kibendi chochote, alisema Mama Diamond.

Mama huyo aliyaweka hayo hadharani jana alipokuwa akizungumza katika kipindi cha XXL cha Clouds Fm ambapo alisema yeye anapatana na Zari ambaye ndiye mkwe wake anayemfahamu na hapatani na Mobeto.

“Napatana naye, mi napatanaga na mtu? Mi mwenyewe nuksi kila mtu ananiona nuksi, nitapatana naye mimi wa nini? 

Akizungumzia madai kuwa Diamond amemnunulia Mobeto gari aina ya Rav4, mama Diamond alisema hayo si ya kweli kwa sababu mobeto ana kazi zake na hivyo anaweza kujinunulia gari lake mwenyewe.

“Basi atakuwa ana hela za mchezo kila mtu kumnunulia gari, kila mtu akinunua gari kanunuliwa na Nasib,.. Hamisa si ana mambo yake, kwani hawezi kununua gari? Mpaka anunuliwe na Nasib?



Mara kadhaa Diamond Platnumz amekuwa akihusishwa kutoka kimapenzi na mwanamitindo, Hamisa Mobeto, na hata wakati fulani ikazua utata baada kudaiwa kukutwa hereni chumbani wak Diamond