Askofu wa Kanisa La Kiinjili La Kilutheri Tanzania Daktari Emmanuel Joseph Makala amekemea vikali hali ya mauaji inayoendelea nchini inayosababishwa na wivu wa mapenzi na kuwaomba akina mama kuwasaidia akina baba kuondokana na huu ugonjwa unaolitesa Taifa.
Askofu Makala ameyasema hayo katika ibada ya Jumapili ya tarehe 12/06/2022 katika Kanisa La Kiinjili La Kilutheri Tanzania Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria usharika wa Ebenezer Kanisa Kuu Shinyanga, ibada iliyoambatana na tukio la kumpongeza aliyekuwa Msaidizi wa askofu na Dean wa Kanisa kuu mchungaji Trafaina Assery Nkya kwa utumishi wake katika usharika huo.
Askofu Makala alisema mauaji yanayoendelea nchini kwa sasa kwa asilimia kubwa yanasababishwa na wivu wa kimapenzi jambo ambalo sheria za nchi zinakataa na vitabu vya dini vinakataa kutoa uhai wa mtu.
"Kazi ya injili pekee ndio inaweza kupunguza mauaji. Lakini kuna ugonjwa mwingine umezuka huu ugonjwa hauna cha kijijini wala mjini, na huu ni ugonjwa wa wivu wa mapenzi. Huu ugonjwa hauna cha kijijini wala mjini."
"Tatizo la wivu wa mapenzi kwa sasa ndio ugonjwa mpya sasa zaidi ya magonjwa mengine kama Corona na magonjwa mengine"
Na mimi sasa simung'unyi maneno tatizo hilo ni kubwa sana na hapa Shinyanga liko juu. Ila tu , sasa hili nalisema kina baba msichukie, mimi nawapongeza akina mama kwa sababu kwa jinsi tulivyoumbwa kina mama wana uwezo mkubwa wa kubeba mambo mioyoni mwao na familia zikabaki, nalisema hili kwa utafiti na kwa kuamini, nyumba nyingi zimesimama kwa sababu ya akina mama." Alisema Askofu Makala
Askofu Makala aliongeza kuwa akina mama wengi wanawajua wanaume wao kwa undani
"Kina mama wanatujua, wanatujua sana na wanatuvumilia mno na unaweza ukakaa miaka kumi uko nae lakini amenyamaza tu."
"Sasa ninyi akina mama wahurumieni hawa wanaume, kwa sababu wanaume wana kesi moja na hili nalisema mara nyingi sana silionei aibu kwanza nimeshazeeka" alisisitiza Askofu Makala
Askofu Makala alisisitiza kuwa, wanaume hawana kifua cha kubeba mambo mazito hususani yanayohusiana na mapenzi ndio maana wanaongoza kwa kuua wanawake zao ila wanawake wao wana uwezo wa kuvumilia
"Mwanamke anaweza akagundua nyendo zako na akweza kuendelea kukaa na wewe ila yeye
mwanaume akiona hata meseji kwenye simu ya mwanamke I love You " kila kitu kinalala hata meseji tu hautafanya kazi."
"Kina baba wengi ndio wameua kwenye hili swala la mapenzi na wameua kwa sababu hawana uwezo wa kubeba kwamba kuna mwenzangu nae anaingia hapo"
Hivi karibuni hapa nchini kumekuwa na matukio mengi ya mauaji ambayo yanasababishwa na wivu wa kimapenzi
Isaac Masengwa - Masengwa Blog
0 Comments