DEREVA WA GARI LA TAKA AUAWA KWA KUPIGWA RISASI SITA AKIPAKIA TAKA

Dereva wa lori la takataka amepigwa risasi na kuuawa akisubiri gari lake kujazwa na taka. Picha: Global Grid.

Dereva huyo ambaye alitambuliwa tu kwa jina Maina alikuwa akiendesha gari lililopewa kandarasi na Mamlaka ya Barabara Kuu nchini (KENHA) kubeba takataka mwenye barabara hiyo kisa hicho kilipotokea mwendo wa saa nne usiku.


Polisi na walioshuhudia walisema mwendazake alipigwa risasi sita na jamaa ambaye alikuwa amejihami na bunduki aina ya AK47.

Maina alikuwa ameendesha lori hilo hadi Handaki ya Utalii na kuliegesha hapo akisubiri lijazwe kwa taka gari dogo aina ya salon liliposimama nyuma ya lori hilo.

Walioshuhudia wanasema kuwa mwanamume mmoja aliruka kutoka kwa gari hilo na kutembea hadi alipokuwa Maina, kumpiga risasi mara sita, kabla ya kukimbia kwenye gari lao na kutoroka kwa spidi.

Wanaume wengine sita ambao walikuwa wakijaza gari hilo kwa takataka hawakujeruhiwa katika shambulizi hilo.

Kikosi cha polisi kilitembelea eneo hilo na kukusanya mabaki sita ya risasi na kuwahoji wahudumu wengine waliosema kuwa walikuwa wamechukua takataka hizo kutoka katikati mwa jiji na walikuwa wakielekea upande wa Kasarani.

Walioshuhudia pia wanasema gari hilo dogo lilikuwa limefuata lori hilo kutoka katikati mwa jiji huku mkuu wa polisi eneo la Starehe William Sirengo akisema kuwa wangali kubaini kiini cha mauaji hayo.

Polisi walipeleka mwili huo katika makafani huku uchunguzi ukianzishwa.

Post a Comment

0 Comments