KADA WA CHADEMA ATINGA MTAANI KUDAI KATIBA MPYA

Kada wa Chama cha Domokrasia na Maendeleo (Chadema) wilayani Sengerema mkoa wa Mwanza, Frank Obwere (33) ameingia mtaani kuhamasisha wananchi kudai Katiba mpya.

Kada huyo amepita mtaani akiwa peke yake leo Jumatatu Juni 7, 2022 huku akiwaambia wananchi kuwa anatekeleza ajenda ya Chadema ya kudai Katiba mpya.

Amesema Katiba hiyo ikipatikana itakuwa suluhusho la matatizo ya Watanzania katika nyanja za siasa na kupata demokrasia ya kweli.

"Mimi nimeingia mtaani kudai Katiba mpya wewe uko wapi tuungane pamoja kudai Katiba mpya tutafanikiwa" amesema Obwere.

Mkazi wa Sengerema mjini, Anastazia Juma amesema ajenda ya kudai Katiba mpya kwa Watanzania ni njema amabapo amedai kuwa ikipatikana chachu ya maendeleo.

Katibu wa Chadema Jimbo la Sengerema, Paskazia Renatus amesema hamasa inayofanywa na viongozi wa chama hicho wilayani Sengerema inaleta chachu ya Wanachadema kuingia mtaani na kudai Katiba mpya.

Hivi karibuni Mwenyekiti wa Bavicha Taifa, John Pambalu akiwa mkoani Mwanza alikutana na wanachama wa Chadema akiwasisitiza kudai Katiba mpya.

Post a Comment

0 Comments