TUNDU LISU ATOA MSIMAMO WAKE KUHUSU TAREHE YA KURUDI NCHINI

Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu, amesema kwamba mara baada ya Waziri wa Mambo ya Ndani Mhandisi Hamad Masauni, kusema kwamba wale wote walioondoka nchini kwa sababu za kisiasa warudi, yeye na wenzake kwa sasa wataanza kujiandaa kurudi.

Lissu ametoa kauli hiyo hii leo Juni 7, 2022, wakati akizungumza kwenye #EATVSaa1 moja kwa moja kutoka nchini Ubelgiji, licha ya kutotaja tarehe rasmi, amesema kauli ya serikali juu yao ni nzuri hivyo yeye na wenzake watawasiliana na viongozi wao,pamoja na familia zao ili kuona wanarudije n yumbani.

"Siwezi kusema tarehe sasa hivi lakini angalau serikali imesema wazi kwamba tutakuwa salama, na kwahiyo sasa tunaanza taratibu za kurehea nyumbani," amesema Lissu

Chanzo - EATV

Post a Comment

0 Comments