RAIS SAMIA AWALILIA WATU 19 WALIOFARIKI KWA AJALI

Rais Sarnia Suluhu Hassan ameetuma salamu za rambirambi kwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Queen Sendinga kutokana vifo vya vya watu 19 katika ajali iliyotokea Mafinga mkiani Iringa.

Taarifa iliyotolewa leo Ijumaa Juni 10, 2022 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais-Ikulu, ZuhuraYunus imesema kuwa Rais Samia pia anawapa pole wafiwa wote na anaungana na familia katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.

Ajali hiyo imetokea leo katika Wilaya ya Mufindi, mkoani Iringa na kusababisha vifo vya wanaume ne 14, wanawake wanne na mtoto mmoja wa kike.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, ACP Allan Bukumbi ajali hiyo imetokea baada ya basi dogo la abiria aina ya Coaster lililokuwa likisafiri kutoka jijini Dar es Salaam kwenda Iringa liligonga lori lililokuwa limeharibika katika eneo Milo.

Wakati majeruhi wakiwa wanaokolewa lilitokea lori lingine lililopoteza uelekeo na kugonga tena Coaster hiyo pamoja na majeruhi waliokuwa wanaokolewa.

Post a Comment

0 Comments