DENIS NKANE ASEMA ISINGEKUWA SOKA ANGEKUWA MUIGIZAJI, AMTAJA JOHARI KUMPENDA


Katika mahojiano na gazeti flani Denis Nkane ameekeza kuwa ni jambo gani angefanya kama asingecheza soka, Nkane anasema: “Mbali na kuibukia kwenye soka malengo yangu makubwa yalikuwa kuingia kwenye filamu, lakini nilishindwa na kujikuta naangukia kwenye soka, sijutii hili ni mipango ya Mungu.”

“Nilichofanya kwenye soka naamini ningekuwa upande wa filamu pia kungekuwa na kitu nimekiongeza. Mwanadada Blandina Chagula ‘Johari’ ndiye msanii aliyekuwa ananivutia zaidi kutokana na uigizaji pamoja na ndoto yangu kukatika natamani kuonana naye, naamini kuna kitu nitamshirikisha.”

Post a Comment

0 Comments