HAJI MANARA AWAPA SOMO WACHEZAJI WA MPIRA


MSEMAJI wa Klabu ya Yanga, Haji Manara amewataka wachezaji wa Tanzania kutumia vyema mitandao yao ya kijamii kujiingizia kipato cha ziada kama anavyofanya yeye wakati watakapostaafu kucheza mpira.

Manara ameyasema hayo leo wakati akitambulishwa kuwa balozi mpya wa taasisi ya kifedha ya Bayport inayotoa mikopo kwa wafanyakazi wa Serikali.

Manara alisema, fulsa hii anayoipata yeye inatokana na ufanisi wake mkubwa katika mpira wa miguu uliomfanya kujipatia kipato kikubwa kupitia mitandao yake ya kijamii.

"Mimi naweza hata mshahara wangu nisiuchungulie hata kidogo lakini kupitia mitandao yangu ya kijamii napata chochote kitu, na ndio maana Bayport wameona wafanye kazi na Mimi, "amesema Manara.

Manara alisema anatamani kuona wachezaji katika mitandao yao ya kijamii wanapata matangazo ya makampuni mbalimbali na kutambua thamani ya mitandao hiyo ili baadae wasiwe na maisha magumu.

Mwakilishi kutoka Bayport Ngula Cheyoy alisema wammchukua Manara kuwa balozi wao kutokana na namna alivyojijengea heshima kubwa katika mitandao yake ya kijamii.
"Bayport tunafanya kazi kwa kufuata taratibu zote za kibenki lakini ni kwa wafanyakazi wa Serikali tu ila uko mbeleni tutaangalia namna gani ya kuwafikia na wengine,"

"Sasa hivi mfumo wa ukopaji umebadilika sana, unapiga simu tu unapewa mkopo tofauti na zamani mpaka ujaze makaratasi mfumo ambao haukuwa rafiki kutokana na wafanyakazi kuwa sehemu tofautitofauti," alisema Cheyoy.

Post a Comment

0 Comments