YANGA YATAJA TAREHE YA KUZINDUA JEZI MPYA


Baada ya klabu ya yanga kusaini mkataba mnono na kampuni ya kubeti ya Sportpesa hii leo, timu imetangaza kuwa kesho tarehe 28 Julai, 2022 itaazindua jezi zake mpya.

Akiongea na waandishi wa habari, Rais wa timu hiyo Hersi Said amesema kuwa kesho wanakwenda kuzindua jezi ambayo haijawahi kutokea Afrika Mashariki na kati

"Kesho Julai 28, 2022 klabu ya Yanga itatangaza jezi yake mpya kwa ajili ya msimu ujao 2022/2023. Itakuwa ni jezi bora kuliko jezi zote zilizowahi kuwepo yanga"

" Sisi ndio tunaweka standards ya jezi na sisi ndio huwa tunaivuka hiyo standard tuliuoiweka. Ubora wake utakuwa namba moja Tanzania na ukanda wa Afrika Mashariki na kati" Alitamba Hersi

Post a Comment

0 Comments