MAMA MZAZI WA WATOTO MAPACHA WALIOKUWA WAMEUNGANA KISHA WAKATENGANISHWA AFUNGUKA MAZITO YALIYOMSIBU


Ndivyo unavyoweza kusema baada ya Amina Amos (17) mama wa pacha waliotenganishwa Julai mosi mwaka huu kurejea nyumbani baada ya kutoweka kwa takribani mwaka mmoja akiwa hajulikani alipo.

Amina alirejea nyumbani akiwa na ujauzito wa miezi mitano Mei mwaka jana, wakati huo akiwa umri wa miaka 16, huku familia yake ikiwa na walakini kukubali umri wa ujauzito huo kutokana na tumbo lake kuonekana kubwa katika umri mchanga wa mimba.

Amina aliyepitia mateso, kukataliwa na kukashifiwa, alieleza namna anavyopitia kipindi kigumu kutokana na mzazi mwenzake ambaye ni baba wa watoto hao kumtelekeza baada ya kujifungua watoto walioungana.

“Aliniambia kwao hawazaliwi mapacha na kwa kuwa wameungana hiyo ni laana. Tulikuwa na mawasiliano mazuri, ila nilipojifungua tu alipigiwa akaambiwa hakujibu kitu akakata simu. Baadaye nikimpigia kumuomba mahitaji ananifokea, hakuwahi kutoa ushirikiano wowote kwangu,” alimwelezea mzazi mwenzake huyo pasipo kutaja jina huku akitaja umri wake ni miaka 27.

Amina ambaye hakufanya mahojiano ya kina na gazeti hili kutokana na umri wake kuwa mdogo, mama yake Dorica Josiah (35) alizungumza kwa niaba ya binti yake kuelezea safari ya ujauzito huo na changamoto zilizojitokeza awali na baada ya binti yake kujifungua.

“Binti yangu alianza kubadilika alipokuwa kidato cha pili. Ghafla alianza kukataa shule, kutokana na kumshinikiza sana alitoroka nyumbani na kutokomea kusikojulikana,” alianza kuelezea Dorica.

Crediti: Mwananchi 

Post a Comment

0 Comments