YANGA YAFUATA MCHEZAJI ULAYA, AMEWAHI KUCHEZEA NEW CASTLE UNITED


YANGA imemalizana na Bernard Morrison akisaini mkataba wa mwaka mmoja kurejea klabuni kwa masharti kadhaa lakini kuna balaa kubwa wanalifanyia kazi kwa usiri mkubwa.

Yanga imeweka wazi kwamba wanashusha mastaa watano wa kigeni na jina kubwa jingine ni Mrundi Gael Bigirimana.

Ni kiungo ambaye ukihesabu timu alizocheza Ulaya inashtua kidogo lakini Mwanaspoti limejiridhisha kwamba kupitia Cedrick Kaze na wakala wake Yanga inapambana kumshawishi atue Tanzania.

Amepitia klabu kama Coventry City, Newcastle United, Rangers na sasa Glentoran ya Ireland ya Kaskazini. Matajiri wa Yanga, GSM wako katika mazungumzo ya kumrudisha Afrika, Bigirimana ambaye ni tegemeo kwenye timu ya Taifa ya Burundi amewahi kutamba na Newcastle United ya England ambayo anaishabikia Rais mstaafu Jakaya Kikwete.

Faili la usajili mpya wa kocha wa Yanga, Nasreddine Nabi linahitaji kupata kiungo aina ya Gael ambaye anayecheza staili ya ‘box to box’.

Mwanaspoti linafahamu kwamba meneja wa mchezaji huyo ambaye anaishi nchini England anakaribia kukamilisha dili hilo ambalo litakuwa ni usajili wa mwisho kwa Yanga kwa wachezaji wa kigeni.

Post a Comment

0 Comments