MAMA AMFUNGA KAMBA SEHEMU ZA SIRI MTOTO WAKE WA KIUME SHINYANGA

OFISA Ustawi wa Jamii Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga, Swahiba Chemuchemu, ametoa adhabu ya kuripoti ofisini hapo kwa kipindi cha miezi sita kwa Yusph Jackson, mkazi wa Nyashimbi, Kata Mhongolo, baada ya mtoto wake wa kiume mwenye umri wa miaka minne kufungwa kamba sehemu zake za siri.-

Chemuchemu amesema hayo leo Agosti 17, 2022 na kueleza kuwa tukio hilo lilutokea Julai 25, 2022, baada ya kupewa taarifa na majirani wa eneo hilo kuwa mtoto anafanyiwa vitendo vya ukatili na mama yake wa kambo.-

Amesema mtoto huyo alikuwa akifungwa sehemu za siri majira ya usiku na mama yake wa kambo, aitwaye Agnes Ezeckiel (19), aliyekuwa akiishi naye, huku sababu ikielezwa akitaka kujisaidia haja ndogo awe anaongea, asijikojolee kitandani.-

"Baba huyo tumemwambia kila mwezi aje aripoti ofisini, ili tujue maendeleo ya mtoto, tumemkabidhi mbele ya viongozi wa serikali ya mtaa na hatakiwi kuhama eneo hilo kipindi cha miezi sita cha kuchunguza mtoto maisha yake na huyo mke wake tulimpeleka polisi,"amesema Chemuchemu.-

Kwa upande wake, Yusuph Jackson amesema yeye ni mfanyabiashara anayezunguka kwenye magulio na ameeleza kitendo alichokuwa akifanyiwa mtoto alikuwa hakijui.

Chanzo - Habari leo

Post a Comment

0 Comments